Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeendelea kuadhimisha siku kumi na sita (16) za kupinga ukatili wa Kinjisia kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu wakiwemo Wanawake na Vijana
Jana Desemba 08, 2021 ulifanyika Mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi na wakazi wa kata ya Gungu kwa lengo la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza ndani ya Jamii
Mgeni Rasmi wa Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambaye ni Mkuu wa idara ya Mipango na Uchumi Ndugu. Frednand Filimbi aliwataka wakazi wa kata hiyo kupiga vita vitendo vya ukatili vinavyoweza jitokeza kutokana na athari zake na kuhakikisha vitendo hivyo vinaripotiwa katika Uongozi wa Mtaa, Kata, Ofisi za Ustawi wa Jamii na Dawati la Jinsia jeshi la Polisi
Aliwataka wakazi wa kata hiyo kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili kupata elimu itakayowasaidia kupambana na vitendo hivyo kwani kutofanya hivyo mzazi au malezi atakuwa anaendeleza ukatili na hivyo atashitakiwa kwa mjibu wa Sheria
Aidha aliwataka wakazi wa kata hiyo kushiriki shughuli za Maendeleo katika ujenzi wa Miradi mbalimbali inayojengwa katika Kata hiyo ikiwemo miradi ya afya na Ujenzi wa Vyumba vya madarasa
Mwanasheria na Wakili kutoka Shirika la Norwegian Church Aid (NCA) Bi. Rosalia Ntiluhungwa alisema ni kosa kisheria kwa watoto wadogo chini ya Umri wa Miaka kumi na nane (18) kuingizwa na kulazimishwa kuoa au kuolewa kwa Lengo la kujipatia kipato kwa wazazi au walezi
Alisema ukatili Mwingine ni Pamoja na Ukatili wa Kimwili unaohusisha vipigo na Kuchomwa na vitu vyenye ncha kali, Ukatili wa Kihisia kama kutukanwa, ukatili wa Kingono kubakwa na kulawitiwa, Ukatili wa kiuchumi kunyimwa fursa ya kufanya kazi na ukatili wa usafirishaji na utumikishaji wa watoto
Mkutano huo uliandaliwa na Ofisi ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ikishirikiana na BAKAID-Kigoma chini ya Ufadhili wa Shirika la Norwegian Church Aid (NCA) na kauli mbiu ya Mwaka huu Kitaifa ni " Ewe Mwananchi, Komesha ukatili wa Kijinsia sasa"
Zaidi tembelea www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa