Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Emmanuel Maganga jana nov 21, amewataka wahudumu wa afya na maafisa lishe katika halmashauri zote za wilaya mkoani humo kuandaa kazi data ya kuwatambua wanawake wote wenye ujauzito kuanzia ngazi ya mtaa, kitongoji hadi wilaya.
Ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika mafunzo ya kamati za lishe mbili zilikutana pamoja katika ukumbi wa mikutano uliopo ofsi ya katibu tawala mkoa, kamati hizo zilizokutana ilikuwa ni kamati ya mkoa na kamati ya lishe halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji.
Akihutubia kikao hicho mkuu wa mkoa alianza kwa kupiga marufuku tabia za watumishi kuchelewa maeneo ya kazini, na katika vikao mbalimbali vya kiutendaji ambapo alisema jambo hilo halivumiliki katika kuelekea uchumi wa viwanda na ni jambo la utovu wa nidhamu na kuamuru ni marufuku kwa kiongozi kuingia katika kikao wakati mkuu huyo wa mkoa akiwa tayari ameshaingia katika vikao vyake.
Baada ya hapo aliueleza mkutano dhumuni la kukutana katika kikao kazi hicho ikiwa ni kuweka mikakati ya kuimarisha lishe bora kwa mama na mtoto kutoka katika wimbi la udumavu na utapiamlo katika ukuaji.
Aliendelea kueleza moja ya athari zinatokana na ukosefu wa lishe bora kwa watoto chini ya miaka mitano ni udumavu jambo linalofanya hata watoto kufanya vibaya katika kuchangamana na jamii na hata matokeo ya shuleni huku akiendea kueleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa matokeo ya mtihani kwa darasa la saba kuwa mkoa wa pili kutoka mwisho katika mikoa 26 ni matokeo ya udumavu yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora.
Katika kufungua kikao kazi hicho mkuu huyo wa mkoa alitoa maagizo ya kufanyiwa kazi zikiwemo halmashauri zote zilizopo mkoani Kigoma, moja ya maagizo aliyoweza kutoa ni pamoja na wanawake wote wenye ujauzito kutambulika kuanzia ngazi ya mtaa au kitongoji wanapoishi kwa lengo la maafisa lishe ngazi ya mtaa kuwafatilia na kutoa elimu juu ya masuala ya lishe ili kuweza kupata kizazi na watoto wenye uwezo wa juu huku akitoa wito kwa wanawake wote wajawazito kuwa wazi na kukubali kutambulika huku akisema ujauzito sio tukio la siri.
Aliendelea kutoa maagizo kwa afisa lishe mkoa kwa kumtaka mafunzo hayo kuhakikisha yanafanyika kwa wilaya zote zilizopo mkoani hapo ambazo hazikuweza kushiriki mafunzo hayo kwa kuwajengea uwezo wataalamu mbali mbali kuhusiana na masuala ya lishe ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa kizazi cha mkoa wa kigoma .
Aliendelea kutoa maagizo ikiwa ni halmashauri zote kutenga kiasi cha Tsh 1000/= kwa kila mtoto aliyeko chini ya miaka 5 kwa lengo la kuwezesha na kuimalisha elimu ya lishe kwa wazazi wa watoto hao na kuweka mikakati tofauti tofauti kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Katika kutoa maagizo hayo ya lishe alitoa pia wito kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi kufatilia suala la ubora wa vyoo katika halmashauri zote mkoani hapo ambapo alisema “bado tuko nyumakwenye suala la vyoo, baadhi ya watu wanaoishi mwambao mwa ziwa hawana vyoo na wanatumia ziwa kama choo chao hasa kipindi hiki cha mvua, nawaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi kufanya ziara maana iko fedha kwa ajili ya kutembelea vyoo kwa ngazi ya wilaya.”
Baada ya kutoa maagizo hayo mkuu huyo wa mkoa aliwataka washiriki wote wa kikao hichomkuwa na moyo safi na kuweka mikakati ya kuwezesha lishe ina boreka, na kusema mafunzo hayo ni muhimu na mwisho wa siku maagizo hayo yatapimwa na baadae alisema mafunzo hayo yamefunguliwa.
Baada ya hapo mwezeshaji kutoka TAMISEMI aliweza kutoa takwimu kwa mkoa wa Kigoma ambazo zinazosababishwa na athari za lishe duni ambapo alieleza kwa mjibu wa tafiti ya mwaka 2016/2017 iligundulika kwamba 34% ya watoto chini ya miaka 5 mkoani Kigoma wamedumaa, 5% chini ya umri wa miaka 5 ni wakondefu(wamekonda), 4% wana uzito uliopitiliza na 14% wana uzito wa chini ukilinganisha na umri wao.
Mwezeshaji huyo aliendelea kuelezea namna lishe inavyotakiwa kwa makundi yote ya vyakula kuanzia pale mama anapopata mimba hadi mtoto anapofikisha miaka miwili, namna ambavyo mtoto anapaswa kufundishwa katika viashiria vya kusikia , kuona na kutambua sauti.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo aliwataka wataalamu kuanzia ngazi ya mkoa na halmashauri kufanya huduma mbali mbali ikiwemo mazoezi ili kuondoa pia matatizo yatokanayo na lishe kama vitambi na viribatumbo, lakini pia kuwa makini na milo wanayoitumia na kufanya uchunguzi wa kujua matatizo yanayosababishwa na masuala ya lishe chanzo chake ni kipi.
Naye Afisa lishe wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma /ujiji Ndugu. Juma akitoa taarifa ya mafanikio katika halmashauri hizo ameeleza kuwa wameweza kuhudumia mitaa 68 katika kutoa elimu wiki ya unyonyeshaji kwa wanawake katika mambo yahusuyo lishe.
Aliendelea kueleza kuwa vikao vyote vinne vya kamati ya lishe vya mwaka vimeweza kufanyika licha ya changamoto iliyojitokeza ya wahudumu wa afya kutofundishwa kuhusiana na ulishaji wa watoto.
Katika kuhitimisha kikao hicho yapo maazimio yaliyoafikiwa kwa ajili ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuweka mpango mkakati wa lishe kwa kila halmashauri, vikao vya kamati ya lishe kufanyika kwa wakati ikiwa ni pamoja na usimamizi shirikishi, kusimamia ubora na udhibiti na usalama wa Chakula, utoaji wa vitamin “A”, Utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu na kufanya matibabu kwa watoto wenye utapiamlo.
Kikao hicho kilichokamilika majira ya jioni kiliweza kuhudhuliwa na wataalamu kutoka mkoani, wakuu wa wilaya wawili ,mkuu wa wilaya ya Buhigwe na mkuu wa wilaya ya Kigoma, mkurugenzi kutoka halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, na wataalamu kutoka kutoka katika manispaa hiyo, wafadhili wa masuala ya lishe kutoka katika taasisi ya NDELA na wafadhili wa semina hiyo ambao ni IMA World Health.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa