Mkuu wa mkoa mhe. Emmanuel Maganga amewataka madiwani wa halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji wanaoshindwa kufanya kazi kwa weledi kuachia madaraka kutokana kulalamikia masuala ya posho.
Ameyasema hayo leo August 6 katika hotuba aliyoitoa baada ya kumwapisha mkuu wa wilaya ya Buhigwe mhe. Kanali Simon Mahenge na mkuu wa wilaya ya Kasulu mhe. Luteni Kanali Michael Masala katika eneo la mikutano mkoani hapo. Amesema mapato ya halmashauri ya manispaa yapo chini kwa asilimia 43% jambo ambalo ni hatari na kusema wanaokwamisha ni madiwani wanaoleta migogoro na marumbano wanayoyafanya kwa wataalamu waliopo.
Katika sherehe hizo za kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Buhigwe na Kasulu, amewataka pia wakuu wote wa wilaya zote za mkoa wa Kigoma kuwashugulikia kisheria wale wote wanaokwamisha shuguli za ukusanyaji mapato wakiwemo wanasiasa.
Lakini pia amewakumbusha viongozi hao na viongozi wengine wajibu wa kiongozi ikiwa ni pamoja na kukubaliana na mazingira, kuwapenda wananchi , na kutompuuza mtu yeyote ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kuwasikiliza wananchi na kutatua changamoto zao .
Ameendelea kuwataka viongozi hao walioapishwa kuwa watiifu kutokana na kiapo na tamko walilosaini mbele ya wakazi wa mkoa wa Kigoma, huku akisema wenye mamlaka kubwa ni wananchi katika eneo lakini pia ndio wasimamizi wakubwa wa katiba,
“msifanye kazi kwa maonyesho bali fanyeni kazi kwa mjibu wa katiba, sheria,na miongozo, msifanye kazi kwa woga , hakuna mtu yeyote mkubwa zaidi yako wewe mkuu wa wilaya, simameni imara, ila sio kwa ubavu bali kwa kufuata taratibu” ameyasema mkuu wa mkoa katika kusisitiza utekelezaji wa majukumu kwa wakuu wa wilaya hao.
Katika hotuba hiyo mkuu wa mkoa amewataka viongozi na wananchi kuendelea kusimamia kila mmoja majukumu yake katika masuala ya usafi wa mazingira,kuendelea kufanya shuguli za kilimo, biashara wakitumia fursa za masoko yaliyopo nchi jirani Burundi na Rwanda.
Mkuu wa mkoa huyo amepongeza suala la ulinzi na usalama wa mkoa licha ya kusema kuna mapungufu madogo ya mauaji yanayoendelea ya mtu mmoja mmoja huku akiwataka viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa kusimamia na kufanya msako wa wahamiaji haramu, na akiwataka wakazi wa mkoa wa Kigoma kutowahifadhi wahamiaji ambao wanaingia nchini kinyume cha utaratibu.
Akizungumzia suala la vitambulisho vya kitaifa mkuu huyo wa mkoa wananchi wameandikishwa lakini si kila aliyeandikishwa anaweza kupata kitambulisho hicho kutokana na lindi kubwa la wahamiaji haramu na kusema mtu asiyepata kitambulisho na arijiandikisha ajiandae kurudi alipotoka.
Kabla ya hotuba hiyo ya mkuu wa mkoa katibu tawala mkoa ambaye ni mgeni mkoani hapo alijitambulisha kwa wote waliohudhulia sherehe hizo na kumshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kuifanyia kazi kwa weledi na kuomba ushirikiano mkubwa kwa viongozi na wananchi.
Katibu tawala huyo amejitambulisha na kusema yeye ni mtaalamu wa masuala ya mawasiliano na mifumo lakini pia akiwa na uzoefu wa miaka 18 katika usimamizi wa mambo ya kifedha pamoja na mabenki, Amemaliza kwa kuahidi kufanya kazi kwa weledi kwa kusimamia sheria, sera na katiba.
Nao wakuu wa wilaya wakiongea baada ya kuapishwa, mkuu wa wilaya ya Kasulu mhe. Luteni Kanali Michael Masala ameahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na kuwataka wananchi nao kumpa ushirikiano.
Naye mkuu wa wilaya ya Buhigwe mhe. Kanali Simon Mahenge ameahidi ushirikiano wa wananchi wa wilaya hiyo na kuahidi kuwa wazi katika kuijenga wilaya hiyo.
Naye mkuu wa mkoa amehitisha amehitimisha kwa kuwashukuru wote waliohudhulia katika sherehe hizo,na kuwataka kila mmoja kwa nafasi kufanya juhudi kwa kuendeleza mkoa wa Kigoma.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa