Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Thobias Andengenye amewataka watumishi wa serikali waliopo Mkoani hapo kutatua matitizo ya wananchi na kusimamia miradi inayoendelea kujengwa kwa waledi
Ameyasema hayo leo Septemba 9,2020 alipokuwa katika ziara aliyoifanya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kufanya kikao na watumishi wa Manispaaa hiyo pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Akiwa katika Manispaa hiyo ametembelea miradi miwili Mradi wa Ujenzi wa Chanzo cha Maji na Mradi wa Ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya wazazi kituo cha Afya cha Gungu ambapo amejionea hatua za ujenzi wa miradi hiyo ilipofikia
Akiwa katika Mradi wa Ujenzi wa Chanzo cha maji Mkurugenzi wa Maji safi na Maji Taka(KUWASA) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Eng. Jonas Mbike akitoa taarifa ya Amesema ujenzi wa Mradi huo umekamilika kwa asilimia tisini na tatu (93%) ambapo una uwezo wa kuhudumia wakazi 384,501 ambapo kwa sasa kadrio la wakazi wa Manispaa hiyo ni Watu 254,368
Ameendelea kusema mradi huo umeanza kufanya kazi ambapo tayari matanki mapya sita (6) na matanki matatu (3) yaliyokuwepo(zamani) yanaendelea kufanya kazi huku uzalishaji ukiwa ni Lita Million kumi na nane (18,000,000) kwa siku na mahitaji kwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji yakiwa ni Lita Million ishirini na tatu (23,000,000) kwa siku
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa maeneo mengi ya Mji maji yanapatikana kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya makazi ya watu, na kufikia mwezi Oktoba mwaka huu tatizo la maji litakuwa limeisha kutokana na uzalishaji utakao kuwa ukiendelea kwa kuzalisha Lita Million mia moja arobaini na mbili (142,000,000) na mahitaji yakiwa Lita Million ishirini na tatu (123,000,000) ambapo wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wataanza kunufaika na mradi huo pia
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo akipokea taarifa ya Ujenzi wa Jengo la Upasuaji na wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Gungu, Msomaji wa taarifa hiyo na Mtendaji wa Kata ya Gungu Bi. Mwavita Lusovu amesema mapema Mwezi Desemba, 2019 Serikali Kuu ilileta fedha Tsh million Mia mbili (200,000,000)/= kwa ajili ya ukarabati wa Majengo yaliyopo katika kituo hicho cha Afya ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo iliona inafaa katika ujenzi wa majengo mapya hayo
Ameendelea kusema katika ujenzi huo mradi huo umefikia Asilimia Sabini na Tano (75%) ambapo mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha Fedha Tsh Million 263,135,180/= hadi kukamilika kwake, na kiasi cha Tsh Million 63,135,180/= kinatarajiwa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Mwailwa Pangani Amesema kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la wodi ya wazazi na Jengo la Upasuaji kutaondoa usumbufu na ukosefu wa majengo hayo hali itakayosaidia akina Mama kuhudumiwa pindi wanaposhindwa kujifungua kwa njia ya Kawaida
Naye Mkuu wa Mkoa huo amepongeza jitihada na usimamizi uliofanyika katika kusimamia miradi hiyo itakaoweza kuwa manufaa kwa wananchi na Wakazi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku akiwataka Viongozi na Watumishi wa Serikali kuendelea kusimamia miradi kwa weledi
Mkuu huyo wa Mkoa amehitimisha kwa kuendelea kuwataka watumishi wa Umma kuwa waaminifu na waadilifu katika kuwatumikia wananchi na kujenga taswira chanya kwa kupenda shughuli na maeneo wanayofanyia kazi
Mkuu huyo wa mkoa yupo katika ziara ya kutembelea wilaya na Halmashauri zote akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambapo anafanya ziara yake akiwa katika Mavazi yake ya Askari ambapo awali alikuwa katika utumishi katika idara hiyo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa