Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amempongeza na Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya na Shule zilizopokelewa na Halmashauri zote mbili za Wilaya hiyo ikiwa ni katika kupambana na athari za Uviko-19
Pongezi hizo amezitoa Leo October27, 2021 katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wakati wa majumuisho ya ziara ya viongozi wa ALAT-Taifa waliyoifanya katika Manispaa hiyo kwa lengo la kukagua thamani ya miradi inayotekelezwa
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imepokea billion moja na million Mia nane tisini (Tsh 1,890,000,000/=) kwa lengo la Ujenzi wa vyumba vya madarasa sitini na tisa (69) , vituo Shikizi na ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya huku akisema Million Mia tisa sitini (960,000,000/=) zimepokelewa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa arobaini na nane (48)
Aidha amewataka Wakuu wa idara na vitengo ambao ndio Wataalamu kusimamia na kuhakikisha miradi inajengwa katika viwango na kufanya kazi kwa mshikamano na kuepuka urasimu katika ujenzi wa miradi hiyo
Amehitimisha kwa kusema hata mvumilia mtumishi yeyote atakaye chelewesha ujenzi wa miradi hiyo na kutumia fedha vibaya huku akisema msimamizi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake atachukuliwa hatua za kinidhamu
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila amesema Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mbili wapo tayari katika usimamizi wa miradi hiyo na kusema Manispaa ya Kigoma/Ujiji kamati za usimamizi na ufatiliaji wa ujenzi wa madarasa tayari zimeundwa
Picha na video zaidi ingia katika maktaba ya Nchi ya tovuti yetu www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa