Mkuu wa wilaya Ndugu Samsoni Anga juzi ameunda kamati ya kufuatili mpaka unaotenganisha halmashauri ya manispaa ya kigoma ujiji na halmashauri ya wilaya ya Kigoma ili kuondoa migogoro na minongono baina ya viongozi wa halmashauri hizo.
Ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya ushauri wa wilaya (DCC) uliofanyika juz nov 14, katika ukumbi wa halmashauri ya manispaaya Kigoma Ujiji ambapo alikuwa amezikutanisha halmashauri zote mbili , hoja hiyo iliwasilishwa na ofsi ya Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kigoma kama agenda katika kikao hicho.
Akisoma taarifa hiyo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Ndugu. Upendo anasema “kwa mda mrefu halmashauri ya wilaya ya Kigoma imeendelea kufahamu kwamba mpaka unaototenganisha Halmashauri ya Kigoma na manispaa ya Kigoma/Ujiji sehemu ya mwandinga unaopita mto ntovye na kuvuka barabara ya Kigoma-kasulu na kuendelea mto huo hadi relini kasha kufuata reli kuelekea mashariki.”
Aliendelea kuzungumzia chanzo cha mgogoro huo alisema “upimaji uliofanyika awali kisheria ulikosewa kwa kutaja mpaka unaotenganisha halmashauri ya wilaya ya Kigoma na halmashauri ya manispaa ya Kigoma/ Ujiji ni eneo la mwandinga unafuata mto Ntovye na kwenda hadi barabara ya Kigoma-Uvinza, kisha kuelekea mashariki kufuata barabara hiyo ya Kigoma-Uvinza hadi kwenye daraja la mto Mugonya kuelekea kusini kufuata mto mungonya .”
Katika kikao hicho Mkuu wa wilaya aliuliza Naibu meya Athuman Juma Athumani kama mgogoro huo anaufahamu jambo alililosema mgogoro huo haujui na halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji haina mgogoro wowote na Halmashauri ya wilaya ya Kigoma, lakini mipaka iliyodhibitishwa kisheria ndio sahihi na ndio halmashauri inaitambua.
Wakichangia baadhi ya wajumbe katika kikao hicho juu ya mgogoro huo baadhi ya wajumbe akiwemo Frank Ruhasha anasema “mgogoro huo haupo halmashauri ya wilaya ya Kigoma ndio inayoibua mgogoro huo na sharti sheria ifuatwe kama maamuzi ya awali yaliyoamuliwa licha ya watu kuwa na historia tofauti tofauti.”
Naye mkuu wa wilaya akizungumzia mgogoro huo aliwajulisha wajumbe wa kikao hicho kwamba mwenye ardhi ni serikali na serikali imeshatoa maamuzi hivyo wajumbe wote na wakazi wa halmashauri zote mbili waheshimu sheria ambayo tayari imetumika kufanya maamuzi.
Katika hitimisho la mgogoro huo alioufanya aliweza kuunda kamati ya watu 17 kwa ajili ya kufuatilia na kuona mpaka huo kwa makubaliano ya meya na mwenyekiti wa halmashauri hizo mbili ambapo alitaja wajumbe watakao husika katika mpaka huo ni pamoja na Meneja TARURA 1 kutoka katika kila halmashauri, meneja TANROAD 1,Meya wa manispaa ya kigoma ujiji, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma, wakurugenzi wa halmashauri zote, viongozi wa mipango miji kutoka kila halmashauri, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mmoja na wawakilishi wa wananchi 2 kutoka katika kila halmashauri.
Katika kikao hicho cha mashauri agenda zingine zilizowasilishwa kutoka katika halmashauri zote mbili ni pamoja na Taarifa za mapato ya ndani, miradi iliyotekelezwa, ambapo kwa manispaa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi kibirizi iliyogharimu Tsh million 50, ujenzi wa madarasa tisa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi kigoma iliyogharimu Tsh milioni 200, na ujenzi wa madarasa shule ya msingi airport uliogharimu Tsh millioni 60, agenda zingine zilizowasilishwa ni utekelezaji wa kunusuru kaya masikini (TASAF).
Akihitimisha kikao hicho alizitaka halmashauri zote kufanya na kuweka mikakati ya kukuza mapato ya halmashauri ili kuweza kusuka gurumu la maendeleo kwa wakazi wa Kigoma na aliendelea kuwataka watumishi wote kuwa waadilifu katika shughuli za kila siku.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa