Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila jana Januari 05, 2022 alifungua mafunzo ya mpango wa uanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya malezi kwa washiriki ishirini (20) kutoka katika kata tano za Manispaa hiyo
Mafunzo hayo yanatarajia kuendeshwa kwa mda wa siku nne na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi huyo wakishirikiana na wadau wa Maendeleo UNICEF na yanatarajiwa kuhitimishwa Januari 08, 2022
Mkurugenzi huyo Akihutubia katika mafunzo aliwataka washiriki wa mafunzo kuwa makini katika mada zitakazowasilishwa ili kwenda kuwafundisha wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto ili kuwa na jamii yenye maadili
Aidha Mkurugenzi huyo aliwataka washiriki mara baada ya mafunzo kuhakikisha vikundi vya malezi vitakavyoanzishwa vinakuwa endelevu kwa kuvitembelea mara kwa mara na kuwashauri viongozi wa makundi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
Mkurugenzi huyo alisema Mpango huo utaendelea kuboreshwa kwa kufikia kata ambazo hazijashiriki kwa kuongea na wadau wa maendeleo na kutenga mapato ya ndani ili vikundi hivyo vya malezi viweze kufanya kazi kwa kata zote
Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kuwataka washiriki hao kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na uviko-19 ikiwa ni pamoja na kuchoma chanjo huku akiwataka kushiriki Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwaka huu 2022
Kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu. Jabir Majira alisema uanzishwaji wa vikundi vya malezi utasaidia upatikanaji wa kanzi data sahihi ya wazazi na walezi ili kusaidiana katika kutatua changamoto zitokana nazo na malezi
Aliendelea kusema mafunzo haya yanalenga kuwafundisha wawezeshaji watakaohusika katika kuhamasisha wazazi, walezi na wananchi kuanzisha vikundi vya malezi ya watoto katika Kata Bangwe, Kibirizi, Gungu, Mwanga Kaskazini, na Katubuka
Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo Ndugu. Masumbuko Warioba Alisema mara baada ya kupokea mafunzo wapo tayari kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha jamii katika kuanzisha vikundi vya malezi ili kuwa na jamii itakayokuwa na maadili na kuepuka vitendo vya ukatili ndani ya jamii
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa