Na Regina Kalima (Afisa Uhusiano KUWASA)
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye Jana March 06, 2023 alisema kukamilika kwa mradi wa chanzo cha maji Amani Beach kutafanya Mkoa wa Kigoma kufunguka kupitia huduma ya maji na wawekezaji wa viwanda na shughuli mbalimbali za kijamii wajitokeze kwakuwa kuna maji ya kutosha sasa.
Mkuu huyo wa Mkoa aliridhishwa utekekezaji wa mradi wa maji na Serikali kusogeza huduma karibu na Wananchi na kumtua Mama ndoo kichwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji na baadhi ya maeneo ta Wilaya ya Kigoma Vijijini.
Ali zungumza Jana mara baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma kutembelea mradi wa ujenzi wa kitekeo cha maji Amani Beach, Ziwa Tanganyika ambao unawanufaisha wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na maeneo ya Mwandiga, Kalalangabo na Kazegunga
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma Mhandisi Mbike Jones Lyimo amesema uzalishaji wa maji kwa wananchi baada ya kukamilika kwa mradi huo ni lita milioni 24 kwa siku ikiwa ndio mahitaji ya maji kwa sasa wakati uwezo wa mradi ni kuzalisha lita milioni 42 kwa siku na kunufaisha watu 384,000.
Amesema watu wanaopata huduma ya maji imefikia asilimia 90 ya wakazi wote na Serikali inaendelea kuleta fedha ambapo mwaka 2022/2023 kazi ya kuongeza mtandao wa bomba km 90 kwa thamani ya Tsh bilioni 1.7 inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 2023 kwa lengo la kuongeza watu zaidi kupata maji.
Pia ameomba Viongozi hao kuchukua agenda ya kuhamasisha wateja kulipa bili zao kwa wakati, kupambana na watu wasiokuwa waaminifu wanaohujumu miondombinu na wezi wa maji ili kuiwezesha Mamlaka kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa