Na Mwandishi Wetu
Walaamu wa elimu ngazi za Halmashauri Mkoani Kigoma wanaendelea na mafunzo ya Siku tano (05) yaliyoanza siku ya Jumatatu February 20, 2023 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Ijumaa February 24, yakìfanyika katika Ukumbi wa Kasulu Motel
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuwawezesha Viongozi wa Elimu ngazi za Kata kufanya Umoja wa Wazazi na walezi (UWAWA) katika shughuli za ufundishaji na ujifunzaji
Mafunzo hayo yamehusisha makundi ya wataalamu mbalimbali Kutoka ngazi za Wilaya wakiwemo Maafisa elimu, Watakwimu wa elimu, Maafisa elimu -Walemavu, Wadhibiti ubora wa elimu, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Wachumi, Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa habari
Akifungua kikao siku ya Jana February 22, 2023 Mratibu wa Mradi wa Shule Bora Mkoani Kigoma Ndugu. David Mwamalasi aliendelea kuwataka wanasemina Kuzingatia mafunzo kwa lengo la kwenda kuwajengea uwezo Maafisa elimu Kata, Walimu Wakuu, na Wenyeviti wa Kamati za Shule kuunda umoja Wazazi na Walezi (UWAWA) katika kuinua viwango vya Taaluma Shuleni
Mkufunzi wa Kitaifa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndugu. Kelvin Rutaihwa aliwataka Washiriki Kuzingatia mafunzo yanayotolewa kwa lengo la kukuza viwango vya elimu Mkoani hapo kwa kushirikiana na Wazazi
Alisema umoja wa Wazazi na Walezi (UWAWA) wanawajibu wa kufanya na kuhudhuria vikao Shuleni, usimamizi na usomaji wa Wanafunzi nyumbani, kuibua na kuendeleza vipaji vya Wanafunzi pamoja na kuhamasisha uandikishaji, mahudhurio na Mvuko wa Wanafunzi
Aidha alisema utasaidia kamati ya Shule katika utekelezaji wa mpango wa Jumla na maendeleo ya Shule , kusimamia Ustawi , usalama na kusimamia ujumuishi wa Wanafunzi kwa kushughulikia Vitendo vya ukatili, na ukiukwaji wa haki za Watoto na kutatua changamoto Za Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu
Katika Kikao hicho mada mbalimbali ziliendelea kujadiliwa ikiwa ni pamoja na Usimamizi wa rasilimali za Shule, Mapitio ya Matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na la Saba Mkoani Kigoma, na Ushiriki wa Jamii katika ukuzaji wa elimu
Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid ukitekelezwa katika Mikoa tisa ukipokea utaalamu wa kiufundi toka Cambrige Education ikishirikiana na Mashirika ya ADD International, International Rescue Committe (IRC) na Plan International
#SHULEBORA #shulebora @plan_tanzania
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa