Na Mwandishi Wetu
Mshauri wa elimu kutoka taasisi ya British High Commission iliyopo Jijini Dar es salaam Ndugu. Collin Bangay siku ya Ijumaa February 03, 2022 alihitimisha ziara ya siku tatu (03) Mkoani Kigoma akikagua namna mradi wa Shule bora unavyotekelezwa Mkoani hapo
Ziara hiyo ilianza February 01, kwa kufanya vikao na Viongozi ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Shule kwa kuongea na Walimu pamoja na kukagua namna Wanafunzi wanavyoshiriki katika zoezi la ujifunzaji
Desemba 02, Akifanya ziara Halmashauri ya Mji wa Kasulu na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu aliwataka Viongozi wa elimu kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na jamii
Aidha aliwataka viongozi kuendelea kuinua kiwango cha elimu jumuishi kwa kuwatambua watu wenye ulemavu na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa Wanafunzi wote wa kike na wa kiume
Afisa elimu Taaluma Mkoani Kigoma Ndugu. David Mwamalasi alisema Serikali inaendelea kusimamia na kuhakikisha makundi yote wanapata elimu kwa usawa pasipo upendeleo
Alisema Serikali inaendelea kushirikiana na jamii kuinua viwango vya elimu, uwepo wa usalama na usawa katika kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora
Afisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Elestina Chanafi alisema mradi wa Shule bora umewawezesha Wataalamu wa Halmashauri hiyo kufanya utatifiti juu ya sababu inayochangia Wanafunzi kuwa watoro kipindi cha masomo na tayari wameanza kuzitafutia ufumbuzi matokeo ya tafiti hiyo
Mwalimu Mtaaluma wa Shule ya Msingi Mazoezi Kabanga iliyopo Halshauri ya Mji wa Kasulu Anna Dismas alisema katika Shule hiyo Wanafunzi wenye mahitaji maalumu na Walimu wa Shule hiyo kupitia mradi wa Shule bora wamepata mafunzo ya Walimu kazini (MEWAKA) ambayo yamewasaidia katika uboreshaji wa Ufundishaji na ujifunzaji katika Shule hiyo
Mradi wa Shule Bora ni mpango wa elimu wa Serikali ya Tanzania kwa ufadhiri wa Mfuko wa UK aid unaolenga kuunga mkono uboreshaji wa elimu Msingi Tanzania ukiweka mikakati sahihi na kuhakikisha watoto wote wenye ulemavu, wanaoishi katika Mazingira magumu, wasichana na wavulana wanapata elimu bora
Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa ya Kigoma, Pwani, Dodoma, Singida, Tanga, Katavi, Simiyu, Mara na Rukwa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa