Na Mwandishi Wetu
Vijana kutoka familia za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanatarajia kunufaika kwa kuwezeshwa ruzuku ya uzalishaji kupitia mradi wa Vijana Salama (Cash Plus)
Ameyasema hayo Afisa Mradi kutoka TASAF Bi. Esther Kivuyo alipokuwa anatambulisha mradi kwa Wakuu wa idara na Vitengo pamoja na Watendaji wa Mitaa Leo July 21, 2023 katika ukumbi wa Manispaa hiyo
Akitambulisha mradi huo amesema Mradi wa Ujana Salama ( Cash Plus) unatekelezwa katika kipindi cha pili cha awamu ya Tatu ya TASAF ambao utahusisha Vijana walio nje ya Shule (wasiosoma na waliohitimu) walio katika kaya zinazonufaika na Mradi wa TASAF wenye Umri wa miaka 14-19
Licha ya kuwezeshwa ruzuku watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali, elimu ya Afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya Virus vya Ukimwi
Zaidi bofya www.kigomamc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa