Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji ndugu. Emmanuel Katemi jana September 12, mara baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo alikutana na watendaji wa kata na watumishi wa ofisi kuu ya mkurugenzi wa halamshauri katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Msimamizi huyo wa uchaguzi wa serikali za mitaa alikutana nao akiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Pangani kwa lengo la kumtambulisha kwa watendaji hao wa kata na watendaji wengine wa ofisi kuu ya mkurugenzi huyo
Mara baada ya kutambulishwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo aliongea na watendaji hao wa serikali kwa lengo la kuwakabidhi tangazo la majina na mipaka ya mitaa iliyopo katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuifikisha katika ofisi za kata ambapo tangazo hilo wataliotoa leo September 13 kwa mjibu wa ratiba.
Msimamizi wa uchaguzi huo alisema amefanya hivo kwa kuwa ni majukumu yake chini ya kanuni ya 5 ya kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa, Tangazo la serikali Namba 372 la tarehe 26/2/2019 pamoja na kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya kijiji na mwenyekiti wa kitongoji katika mamlaka za miji, tangazo la serikali Namba 374 la Tarehe 26/4/2019 na kwa kuzingatia orodha ya mitaa, vijiji na vitongoji vilivyotangazwa kwenye gazeti la serikali namba 536 la tarehe 19/7/2019.
Aliendelea kuwataka watumishi hao watakaoshiriki katika baadhi ya shughuli hizo za uchaguzi wa serikali za mitaa kumpa ushirikiano na kuwa waadilifu katika utumishi wao na kuzingatia kanuni na miongozo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kila jambo kufanyika kwa wakati kwa kutokana na ratiba iliyopangwa.
Naye afisa uchaguzi wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mrisho Bukuku alisema tayari maandalizi yako vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na baadhi ya vifaa vipo na kwa ajili ya shughuli hiyo huku akisema atawakabidhi watendaji wa kata gundi ya kubandikia tangazo hilo alilolitoa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aliendelea kusema vituo vya kupigia kura vitakuwepo katika taasisi za umma katika mitaa iliyopo huku akisema maeneo ambayo yatawekwa vituo yasiyo na taasisi za umma itakuwa jukumu la kushauriana baina ya msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa na vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi huo.
Nao baadhi ya watendaji kata waliokabidhiwa tangazo la majina na mipaka ya mitaa Ndugu. Amesema wamempongeza msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuteuliwa huku akisema wapo tayari kumpa ushirikiano katika shughuli hiyo itakayofanyika na kumuahidi kufanya kazi hiyo kwa uadilifu.
Msimamizi huyo wa uchaguzi wa serikali za mitaa ameteuliwa kati ya wasimamizi 184 waliochaguliwa nchi nzima kwa mjibu kwa mujibu wa Kifungu 201A, cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 288 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 3 na 6(6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi na Mitaa za Mwaka 2019 zilizotolewa kwa Tangazo la Serikali Namba 371, 171 na 374 ya mwaka 2019.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa