Na Mwandishi Wetu
Wananchi na Watumiaji wa mwalo wa katonga wamejitokeza kushiriki kampeni ya Usafi na usafi wa mwalo huo kwa lengo la uhifadhi wa Mazingira kwa kuondoa taka ngumu zinazotokana na bidhaa za Plastiki
Kampeni hiyo imeanza leo March 15, 2023 katika mwalo wa katonga ukishirikisha Diwani wa Kata ya Bangwe, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji Kata, Wavuvi, Wafanyabiashara wa Mazao ya Uvuvi, Vyama vya uratibu wa mwalo na Wananchi kwa kufanya Usafi
Aidha katika kampeni hiyo Ndugu. Arthur Mugema kutoka Environmental management and economic development organizations (EMEDO) amewataka Wakazi na Watumiaji wa mwalo huo Kuzingatia Usafi kwa kuweka taka ngumu katika eneo lililotengwa
Amesema kuongezeka kwa taka ngumu ziwani kutasababisha kuua mazalia ya Samaki, Magonjwa, na kudidimiza uchumi wa Wavuvi, Wafanyabiashara wa Mazao ya Uvuvi, na Wananchi
Amesema kusambaza taka ngumu katika fukwe/Mialo kutaleta athari hasi katika sekta ya uvuvi, uchumi wa jamii, na usalama wa chakula kitokanacho na protini ya samaki
Takwimu kutoka shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na mazingira(UNEP) zinaonesha kuwa kila mwaka zaidi ya tani milioni kumi na moja (11) za taka za plastiki zimekuwa zikiingia katika vyanzo vya maji hasa Bahari na Maziwa duniani kote. Sehemu kubwa ya taka hizi hutokana na shughuli za kila siku za kiuchumi na kijamii ikiwemo uvuvi, utalii, usafirishaji, na biashara
Tafiti zinaonesha kuwa iwapo hali hii itaendelea bila kudhibitiwa, huenda kukawa na taka nyingi za plastiki kuliko samaki katika maziwa na Bahari ifikapo mwaka 2050.
#tuendeleekulindaziwaletu
#ziwatanganyikaziwalako
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa