Na Mwandishi Wetu
Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji umepitia miradi kumi ( 10) yenye thamani ya zaidi ya fedha za Kitanzania billion moja nukta sita (Tsh 1, 689, 012, 308.80/=) huku Viongozi na Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiridhia utekelezaji wa miradi hiyo
Mapema Asububi ya leo Septemba 30, 2022 akipokea Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Manispaa ya kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma alisema Mwenge wa Uhuru Utakimbizwa Kilomita hamsini (Km 50) katika Manispaa wakati ikipitia miradi
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Ndugu. Sahili Nyanzabara Gerarume akizungumza mara baada ya kukamilika kwa miradi yote amesema wameridhishwa na miradi iliyokagualiwa, kutembelewa na kuzinduliwa huku akiwataka Wataalamu kuendelea kufuata maelekezo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali
Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Ester Mahawe kuendelea kusimamia mapungufu machache yaliyojitokeza katika miradi kama vile kubadilisha Vitasa vya milango katika Shule ya Sekondari Buteko katika ujenzi wa Vyumba vya madarasa vinne (04) kwa gharama ya Tsh 80,000,000/= kutoka Serikali kuu na ubadilishaji wa mabati yaliyotumika katika upauaji wa kichomea taka katika Kituo cha Afya kipya cha Buhanda kinachoendelea kutekelezwa kwa gharama ya Tsh 500,000,000/= ikiwa ni fedha zitokanazo na tozo za Miamala ya simu kutoka Serikali kuu
Mwenge Uhuru umezindua mradi wa Ujenzi wa Mtandao wa maji uliogharimu kiasi cha Tsh 500,000,000/= , Uwekaji wa jiwe la Msingi kayika Ujenzi wa Kituo cha Afya Buhanda unaoendelea kwa gharama ya Tsh 500,000,000/=, Uzinduzi wa Ofisi ya Kata ya Rubuga uliojengwa kwa gharama ya Tsh 47,000,000/= ikiwa ni fedha kutoka Mapato ya ndani
Miradi mingine ni uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa barabara ya Mabatini na Muungano B mita 800 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Tsh 535,000,000/= , na uzinduzi wa vyumba vya madarasa vinne (04) katika Shule ya Sekondari Buteko kwa gharama ya Tsh 80, 000, 000/=
Aidha Mwenge wa Uhuru umezindua klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Buronge, Kukabidhi kwa vyeti katika klabu ya Wapinga dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Buteko, kutembelea Banda la Lishe, kugawa Chakula kwa Waishio na virusi vya ukimwi ikiwa ni pamoja na kupokea Shuhuda katika Kituo cha Afya buhanda
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022 ni " Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo"
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa