Naibu katibu mkuu wa TAMISEMI Tixon Nzunda juzi nov 9 alitembelea miradi wa Local Investment Climate(LIC) inayofadhiliwa na ubarozi wa Dernmark na kuagiza chanzo cha mapato cha mwalo wa kibirizi kikaguliwe kila baada ya miezi mitatu ili kudhibiti na kuboresha upoteaji mapato katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Naibu katibu mkuu huyo alitembelea miradi mitatu ambapo mradi wa kwanza alitembelea eneo la soko la jioni eneo la Mwanga center lililojengwa kwa ufadhili wa ubarozi wa Dernmark afisa biashara wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ndugu. Festo Nashon alitoa taarifa ya namna soko hilo jinsi litakavyokuwa likifanya kazi kwa kusema asubuhi eneo hilo litatumika kama barabara inapofika majira ya jioni barabara hiyo itakuwa ikifungwa pande zote mbili na wakazi wa eneo hilo kuendelea na biashara na aliendelea kusema mwitikio wa wananchi katika kulipokea soko hilo ni mzuri na tayari limekamilika kwa kiasi kikubwa likiwa na miundombinu ya vyoo pia.
Baada ya ukaguzi wa mradi wa soko msafara uliendelea hadi mwalo wa kibirizi ampapo kiongozi huyo alipewa taarifa na Afisa uvuvi ndugu.Azizi namna mwalo huo ulivyoboreshwa ambapo ufadhili huo wa Dernmark uliweza kujenga majengo ya stoo ya kuhifadhia mazao ya samaki na dagaa,kufadhili chanja za kisasa za kuanikia samaki na kujenga pavement ya eneo la mwalo huo na eneo la soko la dagaa na samaki eneo la kibirizi, akiwa katika eneo hilo aliendelea kutembelea makampuni ya usafirishaji ya mazao ya samaki na dagaa, na mitambo ya kuzalishia barafu .
Kiongozi huyo alifanikiwa pia kutembelea kituo cha biashara kilichopo katika manispaa hiyo na kutolewa ufafanuzi na afisa biashara namna kinavyofanya kazi , namna wanafohakikisha ukusanyaji mapato hayapotei na namna wanavyotoa lesseni kwa wafanyabiashara.
Baada ya ziara hiyo Naibu katibu mkuu huyo aliweza kuongea na wataalamu wa manispaa ya Kigoma Ujiji na wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma (wakuu wa idara) katika ukumbi wa manispaa ya Kigoma/ Ujiji, ambapo aliwapongeza wakurugenzi wa halmashauri zote mbili kwa kufanikisha ziara hiyo.
Aliendelea kusema miradi yote aliyotembelea imejengwa kwa viwango vinavyohitajika na kuwataka wataalamu kuiendeleza miradi hiyo kwa ushirikiano mkubwa na kuagiza kituo cha biashara kilichojengwa manispaa ya Kigoma Ujiji kiendelee kufanya kazi na wafanyabiashara kuendelea kuja kupata elimu juu ya masuala ya kibiashara.
Naye katibu mkuu huyo alipongeza ubunifu uliofanyika katika manispaa hiyo katika kuhakikisha vyanzo vipya vya mapato vinapatikana kama ujenzi wa soko la jioni katika manispaa hiyo, amewataka wataalamu kuendelea kuboresha eneo hilo la soko la jioni ili kuleta ufanisi mkubwa katika upatikanaji wa mapato.
Lakini pia alitaka mwalo huo kuendelea kujengwa zaidi ili kufanikisha wavuvi wanapoleta mazao yao nchi kavu na kuwataka wataalamu wa manispaa chini ya mkurugenzi kutafuta wafadhili zaidi wa kujenga eneo la kupakulia mazao hayo ya ziwani kama vile TARURA na wengine wengi.
Naibu katibu mkuu huyo akizungumzia suala la changamoto za vifaa vya kuzalishia barafu, ambapo kuna mashine tatu na mbili zikiwa mbovu amewataka makampuni ya kibiashara yaliyoko hapo kufanya ufadhili ili mashine hiyo zitengemae na kuendeleza ufanisi wa kazi wa kila siku.
Aidha naibu katibu mkuu huyo aliweza kuhoji fedha za mradi wa EQUIEP zilizoweza badilishiwa matumizi halmashauri ina mpango gani wa kuzirejesha, naye mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndg. Mwailwa S. Pangani alisema fedha hizo tayari wameanza kuzirudisha kwa vyanzo vya mapato ya ndani na fedha zinazotolewa kuendeshea idara.
Naibu katibu mkuu alimalizia kwa kuzitaka halmashauri zote kufanya maandalizi mazuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019 na kuwataka wakuu wa idara kufanya kazi kwa ushirikiano , kusimamia sheria, kanuni na maadili bila kupatikana na vitendo viovu kama vile rushwa na kuzitaka halmashauri hizo kuendelea kubuni miradi ya kiuchumi,huduma za jamii kama vile shule na zahanati kuzipa kipaumbele.
Naye mkurugenzi wa halmashauri wa manispaa ya Kigoma/Ujiji aliweza kushukuru kiongozi huyo kwa ziara aliyoifanya katika manispaa hiyo na kusema maagizo aliyoyatoa na ushauri alioutoa utafanyiwa kazi ili kuleta ufanisi mzuri wa utendaji kazi na kuendelea kubuni vyanzo vya mapato vipya na kuhakikisha wanasimamia kwa uzuri suala la ukusanyaji mapato.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa