Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo January 26, 2022 amehutubia Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku akieleza Utekelezaji unaoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya sita katika Manispaa hiyo na Mkoa wa Kigoma katika sekta ya afya
Akihutubia Baraza hilo amesema Serikali ya Awamu ya Sita tayari imeleta fedha zaidi ya Billion 16 Mkoani Kigoma kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya afya na vifaa tiba na tayari Wilaya zote za Mkoa huo ujenzi unaendelea
Amesema fedha za awali kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kigoma Tsh Million 500 tayari zimetolewa huku akilitaka Baraza hilo la Madiwani kufanya uamuzi wa haraka wa eneo ambapo Hospitali hiyo itajengwa
Ametaja Ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) ikiwa ni Ujenzi wa jengo la damu salama kwa gharama ya fedha Kitanzania Million 428, Ujenzi wa Jengo la Mapokezi na Mochwali kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 2.8 , Ujenzi wa Jengo la wagonjwa Mahututi na jengo la dharura kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 1.2 huku akisema tayari fedha za ununuzi wa siti scan Billion 1.6 imetolewa kwa ajili ya Hospitali hiyo
Ameendelea kusema Maboresho na Ujenzi wa Hospitali hiyo ni kwa lengo la kuokoa fedha za Wagonjwa ambao wamekuwa wakipatiwa rufaa za kwenda katika Hospitali zenye huduma za Kibigwa kama vile Bugando, na Mhimbili
Aidha amesema kukamilika kwa Ujenzi huo kutaleta mabadiliko ya huduma za kiafya ikiwemo huduma za Kibigwa kupatikana na kuwahudumia watu wengi zaidi wakiwemo wa Mataifa jirani huku akisema baadhi ya Madkatri Bigwa watahamishiwa katika Hospitali hiyo na wataalamu wengine wakipelekwa masomoni
Amehitimisha kwa kuwataka Madiwani na wataalamu kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo katika ufuatiliaji wa fedha wa Ujenzi wa kituo cha afya kipya katika Manispaa hiyo
Awali Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli akimkaribisha Naibu Waziri aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita katika jitihada za kuwahudumia Wananchi huku akimuomba kiongozi huyo kuleta fedha kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha Afya ili kupanua huduma za afya na kuwa na vituo vya afya vya kutosha na kuendelea kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba na dawa katika Hospitali na Zahanati za Serikali zilizopo katika Manispaa hiyo
Naye Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Shabani Ng'enda Kilumbe akitoa salamu amesema asubuhi amepokea vifaa tiba vitakavyotumika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) vilivyogharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Million 105 ikiwa ni jitihada za Serikali na fedha kutoka kwa wafadhili huku akiipongeza Serikali kwa kuanzisha kambi za kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali hiyo huku akisema tayari Wananchi 914 wamepata huduma za Kibigwa
Kwa taarifa zaidi tembelea, picha na video kuhusu taarifa hiyo tembelea www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa