Na Mwandishi Wetu
Vijana kutoka familia za wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Manispaa ya Kigoma/Ujiji wameendelea kunufaika na mafunzo ya fani mbalimbali kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Standi Nchini (VETA)
Vijana hao zaidi ya hamsini na tatu (53) wanaendelea kupata mafunzo ya fani za Upishi, Mapambo, Udereva, komputa , Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo kwa lengo la kujikwamua na kukuza uchumi katika familia zao na kupata stadi za maisha
Mafunzo hayo yanatolewa kwa ufadhili na ushirikiano wa Taasisi ya elimu Nchini Tanzania, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Standi Nchini (VETA) na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Tayari vijana kumi na tisa (19) kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamekamilisha masomo katika fani mbalimbali ambapo vijana kumi na moja (11) wa fani ya Ubunifu, Ushonaji na Teknolojia ya nguo wamegawiwa cherehani kila mmoja kwa ajili ya kuanza kujitegemea
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa