Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba amepokea vifaa vya afya na elimu kutoka Benki ya NMB na kuvikabidhi.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa Leo May 03, 2025 katika hafla iliyofanyikia katika Kituo cha afya cha ujiji.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni vifaa vya kujifungulia, Viti mbio vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda hamsini (50) kwa Wanafunzi kwa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma vikiwa na thamani zaidi ya fedha za Kitanzania Million arobaini na laki mbili.
Vifaa hivyo vya afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa