Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. David Rwazo amewataka Watumishi kufanya manunuzi kupitia mfumo wa Manunuzi wa kielektroniki ( NeST).
Ameyasema hayo Leo Februari 12, 2024 alipomwakilisha Mkurugenzi kufungua mafunzo ya Siku tatu (03) ya mfumo wa Manunuzi wa kielektroniki ( NeST) yanayofanyikia ukumbi wa Kigoma Social hall yakitolewa na Wataalamu kutoka PPRA.
Amewataka kutumia mafunzo hayo kikamilifu ili kuweza kujifunza na kufahamu vema na kuondokana na changamoto za kimanunuzi huku akisema matumizi ya mfumo wa manunuzi ni takwa la sheria mpya ya ununuzi no.10 ya mwaka 2023.
Mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) yanatolewa kwa Watumishi wa Makao makuu ya Manispaa, Watendaji wa Kata, Walimu na Wataalamu wa afya wa Manispaa hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa