Na Mwandishi Wetu
Walimu wanasihi wa Shule za Msingi na Sekondari Jana Januari 06,2022 wamehitimisha mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza Mashuleni na kuleta athari katika suala la ufundishaji na Ujifunzaji
Mafunzo hayo yaliyofanyika Shule ya Msingi Muungano kwa mda wa siku 7 yamewahusisha Walimu thelathini (30) ambao hutoa ushauri na unasahi kwa wanafunzi wawapo mashuleni katika changamoto mbalimbali ikiwemo taaluma
Kaimu Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga akihitimisha mafunzo hayo alisema vitendo vya ukatili kama vile kubaka, kulawiti, na viboko vimekuwa vikifanyika mashuleni na kuleta athari za mimba katika umri mdogo na maumivu ya kimwili
Alisema Utafiti wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania mwaka 2020 ulionesha kuwa asilimia themanini na tisa (89%) ya vitendo vya kupiga na maumivu ya kimwili vimekuwa vikifanyika mashuleni na utafiti huo ukieleza vitendo vingi hufanyika zaidi kwa shule za vijijini
Aidha alisema kukamilika kwa mafunzo hayo kutaleta athari chanya kwa kuhakikisha adhabu zinazotolewa mashuleni zinatolewa kwa mjibu wa sheria na vitendo vingine kama matusi kwa vikikemewa ili kuwa na Wanafunzi wanaojiamini katika suala la ujifunzaji
Alihitimisha kwa kuwataka Walimu Wakuu Mashuleni kutenga Ofisi za unasihi na malezi na kuhakikisha Wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuripoti vitendo vyote vya ukatili ambavyo vinajitokeza na kuhakikisha taaluma inakuwa kutokana na kupinga vitendo hivyo
Naye afisa Ustawi wa Manispaa hiyo Bi. Agnes Punjila alisema wamewaelimisha Walimu juu ya ulinzi na usalama wa mtoto unaimarishwa ikiwa ni pamoja kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaripotiwa katika mamlaka husika kama ustawi wa Jamii na jeshi la polisi
Aliendelea kusema maeneo mengine waliyoelimisha ni njia sahihi za malezi na kuepuka viboko inapobidi ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha watoto kuwa na uwezo wa kutambua na kukataa wanapofanyiwa vitendo vya ukatili
Mwalimu Philipo James wa Shule ya Sekondari Mwananchi na Mwalimu Magdarena Revokatusi wa Shule ya Msingi Msingeni walisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kupinga na kupambana na vitendo vya ukatili Mashuleni kama vile ngono,viboko na matusi kwa wanafunzi huku wakiwajengea uwezo Wanafunzi kutoa taarifa ya vitendo ambavyo wanaweza kufanyiwa
Kwa mjibu wa Tafiti iliyofanywa na Serikali mwaka 2009 juu ya hali ya ukatili na kutolewa mwaka 2011 ilionyesha wasichana 3 kati ya 10 na Mvulana 1 kati ya 7 walifanyiwa ukatili wa Kingono na asilimia 71 ya Wavulana na asilimia 72 ya wasichana walifanyiwa ukatili wa kimwili na utafiti huo ulibainisha kuwa asilimia sitini (60%) ya ukatili dhidi ya watoto hufanyika majumbani huku asilimia arobaini (40%) ukifanyika mashuleni
Picha na video zaidi tembelea Maktaba ya Tovuti www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa