Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Watumishi kuendelea kutekeleza ujazaji wa Mfumo wa kielekroniki wa usimamizi wa utendaji kazi wa Watumishi wa Umma (PERPMIS).
Ameyasema hayo Leo July 24, 2025 alipofanya kikao na Watumishi wa Manispaa hiyo Wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi wa Makao makuu, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Amesema ujazaji wa PERPMIS ni takwa la Kisheria kwa Watumishi wa Umma huku akiwataka kuendelea kutekeleza Majukumu yao na kujaza kwa ufanisi.
Aidha amewataka kuendelea kuwahudumia na kutatua Changamoto zinazowakabili Wananchi katika maeneo yao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa