Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji Siku ya Ijumaa June 17, 2022 ilipokea vifaa vya usafi kutoka kwa wadau wa Maendeleo zikiwemo pikipiki sita (6) za miguu mitatu sita vyenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia mbili (Tsh Million 200) kwa lengo la kuendeleza Usafi wa Mji
Vifaa hivyo vilipokelewa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Bi. Lucia Chingulu kutoka kwa uongozi wa Mradi wa Lake Tanganyika Water Management (LATAWAMA) unaotekeleza Shughuli zake kupitia shirika la lisilo la Kiserikali la ENABEL linanofadhiliwa na nchi za Umoja wa Ulaya (EU)
Akipokea vifaa hivyo Kaimu Katibu Tawala huyo aliwapongeza wafadhili hao kwa jitihada ambazo wamekuwa wakifanya kuhakikisha Manispaa ya Kigoma/Ujiji inakuwa safi kupitia vifaa ambavyo wamekuwa wakivitoa mara kwa mara huku akiwataka Wataalamu kusimamia vifaa hivyo na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta tija katika usafi wa Mji
Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli katika makabidhiano hayo alivitaka vikundi vya usafi vitakavyokabidhiwa vifaa hivyo kuhakikisha wanalinda na kuvitunza huku usafi wa Mji ukiimalishwa
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kajanja Lawi aliwashukuru wadau hao wa Maendeleo kwa vifaa walivyovitoa huku akisema vifaa hivyo vitasimamiwa kwa ukamilifu ambapo na kusema pikipiki hizo zitatumika na madereva wake kukusanyia taka Mtaani huku zikitoa ajira na kuongeza Mapato ya Wananchi na Halmashauri
Mkurugenzi wa Shirika la Utunzaji Mazingira (LATAWAMA) Ndugu. Didier Cadelli alisema vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni Ukarabati wa lori moja la Halmashauri, ununuzi wa Mashine za Kukusanyia Mapato (POS) kumi na tano (15) , Viźimba vya kuwekea taka viwili (2), na vifaa vya kinga binafsi(PPE) ,
Aliendelea kusema katika kuhakikisha vifaa hivyo vinaimarishwa kama vile Pikipiki za Miguu mitatu mafunzo yametolewa kwa madereva kutoka chuo cha VETA Kigoma
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa