Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion moja na milion mia moja arobaini na Sita (Tsh 1, 146, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa lengo la Ujenzi wa vyumba vya madarasa hamsini na saba (57) ikiwa ni Maandalizi na Mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa Mwaka 2023
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe Leo October 10, 2022 amefanya kikao na Viongozi na Wasimamizi wa miradi ya elimu kwa lengo la kuweka mikakati namna utekelezaji na ujenzi wa madarasa hayo kwa viwango vilivyo bora
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Wakurugenzi, Watendaji Kata, na Wakuu wa Shule kuzingatia weredi katika kuchagua Mafundi watakaoomba kazi hizo za Ujenzi wa madarasa na kuepuka Mafundi wasio kuwa waadilifu
Aidha amewataka Wahandisi kusimamia mpango wa Ujenzi (BOQ) na Maafisa manunuzi kuhakikisha mipango ya manunuzi haicheleweshi utekelezaji na ujenzi wa madarasa hayo
Aidha amewataka Waheshimiwa Madiwani wenye miradi kutambulisha miradi hiyo kwa Wananchi kwa kufanya mikutano ili kuwa na uelewa juu ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao
Naibu Meya wa Manispaa ya Kigoma /Ujiji Mhe. Mgeni Kakolwa ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuleta fedha za Maendeleo katika Manispaa hiyo kwa lengo la kuboresha miundombinu na jukuza taaluma
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Evansi Mdee amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari imeshafanya vikao na Wakuu wa idara wanaohusika na ujenzi wa Madarasa hayo wakiwemo Maafisa elimu, Wahandisi na Maafisa manunuzi kwa lengo la kuhakikisha miundombinu itakayojengwa inakuwa bora na kuwa na Usimamizi na ufautiliaji wa mara kwa mara
Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Katibu Tawala wa Wilaya, Naibu Meya na Mwenyekiti wa Halmasharuri ya Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji Kata, Waratibu elimu Kata na Wakuu wa Shule
Kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilitekeleza Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa arobaini na nane (48) yaliyogharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Million mia tisa sitini (Tsh 960,000,000/=) ikiwa ni fedha zilizotoka Serikali Kuu
Kwa taarifa zaidi endelea kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ili kupata taarifa zaidi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa