Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hassan Rugwa Jana August 29, alifanya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa ni maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024.
Kiongozi huyo alikagua miradi inayotarajiwa kutembelewa, kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu.
Kiongozi huyo alikagua ujenzi wa Zahanati mpya Kata ya Kitongoni, Ujenzi wa nyumba ya Walimu Shule ya Sekondari Businde, Ujenzi uliokamilika Ofisi ya Kata ya Buhanda, Chanzo cha Maji Kibirizi, Mradi wa Vijana Kata ya Gungu, na Ujenzi wa barabara ya Stanley kwa kiwango cha lami Kata ya Kigoma.
Kiongozi huyo alipongeza namna ambavyo maandalizi yanaendelea huku akiitaka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuendelea kusimamia kukamilishwa kwa miradi inayoendelea kujengwa ili kuanza kutoa kutoa huduma kwa Wananchi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinatarajia kukimbizwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Septemba 16, Mwaka huu na kauli mbiu ni "Tunza Mazingira na Shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa