Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Thobias Adengenye imefanya ziara ya Kukagua miradi inayotarajiwa kutembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2023
Kamati hiyo imefanya ziara ikitembelea miradi iliyotekelezwa na inayotekezwa kwa Mapato ya ndani ikiwemo Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Buhanda, Katubuka, na Ujenzi wa Zahanati Kata ya Machinjioni na Shamba darasa la Mboga mboga Shule ya Sekondari Kigoma
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa Shule ya Msingi Katubuka kupitia mradi wa BOOST, Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa tanki la maji lilipo Kamala Bangwe
Mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa Mkoani Kigoma Agusti 16, Mwaka huu na kupokelewa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Augusti 22, na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai, na Uchumi wa Taifa"
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa