Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amelitaka Jeshi la Polisi kushugulika na madereva boda boda wanaovunja Sheria za barabarani badala ya kushughulika na vyombo vyao.
Aliyasema hayo Jana Januari 16, 2025 katika ukumbi wa Angilikana alipofanya Mkutano na Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda kwa lengo la kutatua Changamoto zinazowakabili.
Alilitaka Jeshi la Polisi kushughulika madereva ambao wanakiuka taratibu na Sheria za barabarani na kuacha ukamataji holela holela kama vile kwenye vituo vya mafuta huku akiwataka Maafisa usafirishaji maarufu bodaboda kuzingatia Sheria katika Majukumu yao ya Kila Siku ya usafirishaj.
Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Kigoma Ujiji wanafanya Kikao cha pili mara baada ya kikao cha Kwanza kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kikifanyika Uwanja wa Kawawa January 10, Mwaka huu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa