Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP(Mst) Balozi Simon Sirro Asubuhi ya Leo Agosti 8,2025 ametembelea banda la Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji yanayohitimishwa katika viwanja vya Fatuma Mwasa Manispaa ya Tabora.
Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa namna ambavyo imeendelea kuweka Mazingira wezeshi kwa Wakulima, Wafugaji na Wajasiriamali katika kutekeleza Shughuli zao za Kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Sirro ndiye mgeni rasmi kwenye kilele cha Maadhimisho hayo Kanda ya Magharibi inayohusisha mikoa ya Kigoma na Tabora..
Kauli mbiu ya Nane Nane Mwaka huu ni "Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa