Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Adengenye Leo January 20, 2023 ameagiza Wasimamizi wa elimu ngazi ya Halmashauri kushirikiana na kamati za Wazazi Shuleni kuhakikisha Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata chakula katika kipindi chote cha masomo wawapo shuleni
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu ngazi ya Mkoa kilichofanyikia Ukumbi wa NNSF uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikishirikisha Wataalamu wa Sekratarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Meya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi, Wakuu wa idara, Maafisa elimu Kata, na Walimu Wakuu wa Shule za Mkoa wa Kigoma
Akihutubia katika kikao hicho Mkuu huyo wa Mkoa amesema Wanafunzi hawawezi kufanya vizuri kitaaluma kama watakuwa wakishiriki zoezi la ujifunzaji wakiwa na njaa
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka kamati za Wazazi kwa kila Shule ziratibu namna Wanafunzi watakavyopata chakula cha pamoja kwa kuwahusisha Wazazi wanashiriki na kuamua chakula gani kitumike mashuleni
Aidha amewataka Wasimamizi wa elimu ngazi ya Mkoa,Halmashauri, Kata na Shule kufanya tathimini ya Matokeo ya mitihani ndani ya siku thelathini (30) Mara baada ya matokeo ya mitihani kutolewa ili kubaini changamoto na mafanikio
Ameendelea kuwataka Wazazi wote wenye Watoto waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza na Wanafunzi wa darasa la kwanza wanaripoti Shuleni kwa mda uliopangwa
Awali akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za elimu kwa Mwaka 2022 Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Bi. Paulina NdigezĂ amesema hadi sasa Shule zinazotoa chakula kwa Mkoa wa Kigoma ni Shule 156 za Msingi kati ya 708 na Shule za Sekondari 43 kati ya Shule 218 ambazo kitaaluma zimekuwa zikifanya vizuri katika ufaulu wa mitihani
Mkoa wa Kigoma Kwa Mwaka 2022 ulipokea fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 12. 9/= kwa Ujenzi wa Madarasa 549 , huku Million 624.6/= ikipokelewa kwa Ukamilishaji wa maboma ya madarasa
Aidha kupitia mradi wa Sequip Mkoa wa Kigoma umepokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 5. 2/= kwa Ujenzi wa Shule mpya za Sekondari kwa Kata ambazo awali hazikuwa na Shule za Sekondari
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa