Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatambua mchango wa boda boda katika sekta ya usafirishaji na kuinua uchumi Nchini.
Ameyasema hayo Leo Januari 10, 2025 alipofanya mkutano na madereva boda boda katika uwanja wa Kawawa.
Ametoa zuio kwa baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa katika kusimamia dereva bodaboda ikiwa ni pamoja na kuwachapa fimbo huku akitaka madereva hao kufuata Sheria za barabara wawapo kazini.
Mkuu huyo wa Wilaya amefanya kikao na dereva bodaboda hao mara baada ya Siku ya Jana kuandamana wakipinga namna ambavyo Jeshi la Polisi limekuwa likitumia nguvu kubwa katika kuwadhibiti.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa