Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) imegawa vifaa vya kujifunzia kwa Shule za Msingi kumi (10) Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa zaidi ya Wanafunzi Mia tano themanini na Saba (587).
Vifaa hivyo vimegawiwa kwa Wanafunzi ambao hawakuwahi Kusoma kwa sababu ya utoro, kuacha Shule, na Sababu zingine na kwa sasa wapo katika Mfumo rasmi na katika masomo ya MEMKWA ya kujenga stadi za Kusoma, Kuandika na kuhesabu.
Wanafunzi hao wamegawiwa Mabegi, Daftari na vifaa vingine kwa Shule ya Msingi Benjamini Mkapa, Bangwe, Kibirizi, Bushabani, Buronge, Gungu, Butunga, Mwasenga, Azimio na Shule ya Msingi Mbano.
Jana May 10, 2024 Akizungumza katika zoezi la Kuwakabidhi vifaa hivyo Afisa elimu idara ya elimu Awali na Msingi Ndugu. Richard Mtauka aliishukuru Serikali kwa namna ambavyo imefanikisha Watoto ambao awali waliacha masomo kutokana na sababu mbalimbali na tayari wamerejea katika masomo.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa