Manispaa ya Kigoma ujiji kupitia ofsi ya Mkurugenzi ikishikirikiana na wafanyabiashara wa soko la Nazareth juzi Desember 9. Walifanya usafi katika soko la Nazareth ikiwa ni kusheherekea miaka 57 ya Tanzania kujipata uhuru kutoka katika utawala wa kikoloni.
Usafi huo uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Ndugu. Brown Nziku akiwa na wataalamu mbalimbali kutoka katika ofsi yake ambapo usafi ulifanyika katika eneo la kukusanyia taka, usafi wa mitalo, kufyeka maeneo yenye nyasi ndefu na kufagia eneo la vichanja vya kuwekea bidhaa.
Baada ya usafi huo uliochukua masaa manne ukifanyika, kaimu Mkurugenzi aliongea na wafanyabiashara wa soko hilo akiwashukuru kwa ushirikiano mzuri waliouonesha katika kusheherekea miaka hamsini na saba ya uhuru kwa kufanya usafi ikiwa ni jambo la kuepuka magonjwa ya mlipuko hasa kipindi hiki cha mvua, na kufanya mazingira kuonekana katika hali ya usafi.
Kaimu mkurugenzi huyo aliwataka wafanyiashara wa soko hilo kuhakikisha pindi wanapokusanya taka kuziweka katika vizimba vilivyopo katika soko hilo licha ya baaadhi ya wenye tabia zisizofaa kuweka uchafu huo nje ya vizimba jambo linaloleta sura mbaya ya uchafu.
Kaimu mkurugenzi huyo Ndugu. Brown Nziku akiendelea kuongea na wafanyabiashara aligundua wafanyabishara wengi kutodai risti pindi wanapotoa kodi jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya soko hilo pamoja na kuhafifisha mapato ya halmashauri, aligundua hilo baada ya akina mama kupaza sauti wakimwambia wanadaiwa kodi lakini hawapewi risti.
Naye kaimu mkurugenzi akijibu suala hilo alimtaka mzabuni anayeshugulika na ushuru wa soko hilo kuhakikisha pindi anapokusanya kodi kuto a risti halali na kuwataka wafanya biashara wote kuhakikisha wanadai risti ili kuendeleza ufanisi wa soko hilo na ustawi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Naye mkuu wa kitengo cha usafi na mazingira Ndugu Mashaka Juma aliendelea kuwasisitiza wafanyabiashara wa soko hilo kuhakikisha kuendelea kufanya usafi kila mara na kutosubili matukio kama hayo tu ya kitaifa huku akiwataka kukusanya taka katika vizimba na kusema ofsi yake itahakikisha taka hizo zinatolewa kwa wakati.
Naye mwenyekiti wa soko hilo aliweza kupongeza ofsi ya mkurugenzi kwa moyo waliouonesha kusheherekea sikukuku ya uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi katika soko hilo huku akimuhakikishia kaimu mkurugenzi huyo usafi wa soko hilo utaendelea kila mara mara na wafanyabiashara wataendelea kudai risti pindi wanapolipa kodi ili kuendeleza ustawi wa halmashauri .
Katika kusheherekea uhuru huo ni baada ya harakati za baba wa Taifa mwl. Julius Kambarage Nyerere ambapo December 9, 1961 alilipatia uhuru taifa la Tanzania uhuru kutoka katika mikono ya wakoloni ambapo baada ya hapo alipigania suala la elimu kwa kila Mtanzania, na afya bora na sasa tuko katika utawala wa Rais awamu ya tano Dr.John Pombe Magufuli ambapo licha ya kupambana na ufisadi anataka kuhakikisha nchi inakuwa Tanzania ya viwanda.
Picha zaidi za tukio hili nenda katika maktaba ya picha.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa