Na Mwandishi Wetu
Shule Mpya ya Sekondari iliyopo Burega Kata ya Buzebazeba Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatarajia kupokea Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Mwaka huu 2026.
Shule hiyo itapokea Wanafunzi Mia moja na sitini (160) baada ya miundombinu ya madarasa manne (04) ya ghorofa (Ground floor) kukamilika, viti na meza za Wanafunzi na Walimu zikiwa tayari.
Miundombinu mingine ambayo imeshakamilika ni Jengo la Maabara, Jengo la TEHAMA, Jengo la Maktaba, na Jengo la Utawala.
Ujenzi wa Shule hiyo unatekelezwa na Serikali Kuu kupitia Mradi wa SEQUIP kwa fedha za Kitanzania zaidi ya Million mia sita (Tsh 603, 890,563.00/=) na fedha kutoka Mapato ya ndani inayoendeleza Ujenzi wa miundombinu ya madarasa ya ghorofa.
Serikali ya Awamu ya sita imeendelea kuimarisha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia na Shule kuwa taasisi salama na jumuishi zinazoweka kipaumbele kwenye Ustawi na fursa sawa kwa Watoto na Vijana wote ili kuwa na wahitimu wenye ujuzi stahiki na uwezo wa kushindana na kufanikiwa katika Soko la Ajira Kimataifa.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa