Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha za Kitanzania zaidi ya Billion Moja (Tsh 1, 467, 200,000/=) Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la uboreshaji na ujenzi wa Miundombinu kwa Shule za Msingi
Serikali imeleta fedha hizo kupitia mradi wa BOOST unaotekelezwa Nchini katika uboreshaji wa Miundombinu ya elimu
Katika fedha zilizopokelewa Manispaa ya Kigoma/Ujiji jumla ya Shule tatu (03) mpya zinatarajiwa kujengwa kwa gharama ya Tsh 922,600,000/=, Ujenzi wa Madarasa kumi na sita (16) kwa gharama ya Tsh 416,000,000/=, Ujenzi wa madarasa 2 ya elimu ya awali ya mfano kwa gharama ya Tsh 71,800,000/=, Ujenzi wa darasa 1 la elimu maalumu Tsh 26,000,000/=, na Ujenzi wa matundu kumi na nne (14) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 30,800,00/=
Shule zinazotarajiwa kunufaika na mradi wa BOOST ni pamoja na Ujenzi wa Shule mpya Kiheba iliyopo Kibirizi kwa gharama ya Tsh 561,100,000/= na Ujenzi wa Shule mpya ya Kibirizi kwa gharama ya Tsh 361,500,000/=
Shule ya Msingi Katubuka inatarajiwa kujengwa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, Ujenzi wa darasa moja (01) la Wanafunzi wenye Mahitaji maalumu kwa gharama ya Tsh 26,000,000/= na ujenzi wa Matundu matatu (03) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 6,600,000/=
Shule ya Msingi Kabingo inayotarajia kutekeleza ujenzi wa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, na Ujenzi wa matundu manne (04) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 8,800,000/=,
Aidha Shule ya Msingi Kipampa inatarajiwa kunufaika na ujenzi wa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, na Ujenzi wa matundu matatu (03) ya Vyoo kwa gharama ya Tsh 6,600,000/=
Shule ya Msingi Butunga inatarajiwa kujengwa madarasa manne (04) kwa gharama ya Tsh 104,000,000/=, Ujenzi wa madarasa mawili (02) ya awali ya Mfano kwa gharama ya Tsh 71,800,000/=, na Ujenzi wa matundu manne (04) ya vyoo kwa gharama ya Tsh 8,800,000/=
Endelea kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa