Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwa lengo la kuhamasisha jamii kuhusu haki na ustawi wa Watoto.
Maadhimisho hayo yamefanyika Leo June 16, 2025 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Katubuka yakihudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Taasisi mbalimbali, Wazazi na Walezi Mgeni rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Mganwa Nzota.
Akihutubia Mkutano Mgeni rasmi ametoa wito kwa jamii kuimarisha usalama na ulinzi wa mtoto katika kila hatua ya malezi na makuzi.
Amesema Jamii inapaswa kuendelea kulinda haki za Watoto na kuwalinda dhidi ya vitendo vya Ukatili kwa kuzingatia Haki za kuishi, kuendelezwa kielimu, na kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema Serikali imeendelea kutekeleza upatikanaji wa elimu bure kwa Watoto Wote, uimarishaji wa huduma za afya , ulinzi na Usalama kwa kuimarisha madawati ya Ustawi wa Jamii.
Kauli Mbiu katika maadhimisho ya Mwaka huu ni" Haki za Mtoto, Tulipotoka, Tulipo na tunapoelekea".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa