Na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa (Mb) amewataka Waheshimiwa madiwani, Wakuu wa idara na Wataalamu mbalimbali wa Wilaya ya Kigoma kusimamia maendeleo ya Wananchi kikamilifu.
Ameyasema hayo Leo Septemba 23, 2023 katika kikao kazi cha Waheshimiwa madiwani na Wataalamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kilichofanyikia ukumbi wa NNSF-Kigoma.
Katika Kikao kazi hicho amewataka viongozi hao kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa fedha kutoka Serikali Kuu na Mapato ya ndani.
Aidha amewataka Wataalamu kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, Kanuni, na Sheria na huku akiwahakikishia Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuwa Serikali itaendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo katika Sekta mbalimbali.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa