Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana May 05, 2023 ilipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ujenzi na matengenezo ya barabara Manispaa ya Kigoma/Ujiji kutoka Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kigoma
Taarifa hiyo iliwasilishwa na Meneja wa TARURA Wilaya ya Kigoma Mhandisi Elias Mutapima kwa utekelezaji wa Mwaka wa fedha 2022/2023 katika Ukumbi wa Manispaa hiyo
Akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji alisema hadi Kufikia Mwezi April, 2023 Wilaya ya Kigoma imepokea kiasi cha Tsh 1,939,754,900/= kwa ajili ya matengenezo ya barabara za Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kiwango cha lami, na Changarawe
Aidha alisema kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 TARURA Wilaya ya Kigoma imeomba kuidhinishiwa kutumia kiasi cha Tsh 4,245,290,000/= kwa kazi za matengenezo ya barabara yenye jumla ya Kilometa 105. 75 Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa