Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) imetoa mipira Mia nne (400) kwa Shule za Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa Miguu kwa Wanafunzi Wavulana na Wasichana.
Mipira hiyo imegawiwa kwa Shule za Msingi kumi (10) ikiwemo Shule ya Msingi Katubuka, Mwenge, Kibirizi, Muungano , Bangwe, Ujiji, Karuta, Burega, Kipampa na Kikungu kila moja ikipata mipira arobaini (40).
Jana May 20, 2023 akikabidhi mipira kwa Walimu na Wanafunzi Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Evans Mdee alishukuru shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) huku akisema Manispaa hiyo itasimamia michezo mashuleni ili kufikia lengo lilokusudiwa.
Awali akitoa taarifa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Abdul Utimbe alisema mipira hiyo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) chini ya mradi wa FIFA Football for Schools.
Alisema lengo la Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji ni kupata wachezaji mahili Mia nne (400) kutoka kwenye Shule hizo kumi (10) na Uratibu wa mradi huo utafanywa Shirikisho ngazi ya Taifa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa