Na Mwandishi Wetu
Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Leo Oktoba 10, 2024 imeendelea na ziara Manispaa ya Kigoma/Ujiji yenye lengo la kukagua maandalizi ya Uandikishaji wa orodha ya Wapiga Kura na Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2024.
Wataalamu hao wamekagua Masanduku ya kupigia Kura yanayotarajiwa kutumika Novemba 27, Mwaka huu pamoja na Vituo vya kujiandikishia kwenye daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina jumla ya Vituo 156 na Zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa linatarajia kuanza Kesho Siku ya Ijumaa Oktoba 11-20, 2024 Saa mbili kamili Asubuhi ambapo pia Vituo vitakuwa vikifungwa Saa kumi na mbili jioni.
#shirikiuchaguziwaserikalizamitaa2024
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa