Na Mwandishi Wetu
Kamati za maafa ambazo pia ni timu za dharura Mkoani Kigoma zimeanza kupata Mafunzo na kujengewa uwezo juu ya masuala ya kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko katika maeno yao.
Mafunzo hayo yameanza kutolewa Jana April 16, 2024 Wilayani Kasulu na Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na Wataalamu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa Wataalamu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kakonko.
Akitoa utangulizi Wakati wa Mafunzo Mkurugenzi wa mradi wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Menejimenti ya Maafa, Sera, Bunge na Uratibu Dr. Salum Manyatta alisema Mafunzo hayo yanatolewa kwa Siku nne (04) kwa Wataalamu wa Sekta Afya, Mifugo, Maliasili, Mazingira, Waratibu wa Maafa, Wataalamu wa Maabara na Wataalamu wa Mawasiliano.
Alisema mafunzo haya yanafanyika chini ya mradi wa Afya moja unaofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na kupitia miongozo na namna kukabiliana na tathimini ya milipuko ya magonjwa, maafa na Majanga.
Mratibu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ambaye ni muepidemiolojia Dr. Justine Assenga alisema mradi wa Afya moja unalenga kutatua Afya za viumbe mbalimbali ikiwemo Afya za Binadamu, Wanyama na Mimea.
Asilimia Sitini (60%) ya magonjwa yanayomuathiri mwanadamu yakiwemo magonjwa ya mlipuko yanatoka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu (Zoonatic disease) kama vile Ebola, Marbug, Kichaa cha Mbwa, Kimeta, na ugonjwa wa Macho Mekundu(Red eyes).
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa