Na Mwandishi Wetu
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini Bi. Mwantum Mgonja amewataka Viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi mdogo kata ya Kasingirima kuepuka vitendo vya vurugu vinavyoweza kusababisha Uchaguzi kutokuwa wa uhuru na haki.
Ameyasema hayo Leo March 19, 2024 alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa ofisini kwake, ambapo Uchaguzi mdogo wa Udiwani unatarajia kufanyika Kesho Siku ya Jumatano March 20, 2024.
Amesema wale waliofanya na waliopanga kufanya vurugu ikibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa, hivyo amesisitiza kuhakikisha wapiga kura wanajitokeza siku ya Kesho katika kuchagua kiongozi wanaomtaka.
Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, SSP-Raphael Msela amesema Jeshi la polisi limejipanga katika kusimamia amani na utulivu katika zoezi hilo la Uchaguzi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa