Na Mwandishi Wetu
Tume ya Haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora inatarajia kufanya Mikutano ya hadhara kwa Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ameyasema hayo Kamishina wa Tume ya Haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora Mhe. Amina Talib Ali Leo Februari 10, 2025 alipofanya mkutano na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Amesema Wataalamu wapo Mkoani Kigoma kutoa elimu kwa Watendaji wa Serikali na kukutana na Wananchi kwa kufanya mikutano ya hadhara ili kutoa ushauri na kupokea malalamiko ya uvunjifu wa haki za binadamu na kuelewa Misingi ya Utawala Bora.
Pia mikutano hiyo itafanyika kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
Amesema mara baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi tume inatoa siku tisini (90) kwa Uongozi wa Mkoa na Wilaya kupata mrejesho na kutoa majibu ya malalamiko ya Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @chraggtanzania
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa