Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba Leo July 24, 2025 amefanya kikao na Watumishi wa mbalimbali ikiwa ni Maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa uhuru katika Manispaa hiyo.
Katika kikao hicho Mkurugenzi huyo amewataka Wananchi na Watumishi kujiandaa kushiriki mbio za Mwenge wa uhuru unatarajia kukimbizwa Katika Manispaa hiyo Septemba 21, Mwaka huu.
Mkurugenzi huyo amesema kwa Mwaka huu Manispaa imejiandaa kufanya vizuri zaidi katika Vigezo vyote na kuwa katika nafasi ya juu ya ushidi Kimkoa, kikanda na Kitaifa kuanzia Vigezo vya Mapokezi, Miradi, na Mkesha kutokana na Hamasa itakayofanyika ikiongozwa na Wananchi.
Aidha amewataka Viongozi kuendelea kutekeleza Majukumu yao na kuwahamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu kuanzia Mapokezi, maeneo ya miradi na uvaaji wa Sare.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa