Na Mwandishi Wetu
Zoezi la Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa linaendelea katika vituo vilivyopo katika Kata na Mitaa kwa Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Serikali inatekeleza zoezi hilo kwa lengo la kulinda Afya za Wananchi kwa kudhibiti na kupambana na kiwango cha Maambukizi ya Ugonjwa huo ikiwa ni 6.6%.
Zoezi la ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwa Wananchi limeandaliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa ushirikiano na
Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria (NMCP) na kutekelezwa katika Mikoa yenye Maambukizo Makubwa ya Ugonjwa wa Malaria Nchini.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @msdtanzania @wizara_afyatz #zeromalaria
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa