Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Katika Kata ya Kipampa unaendelea kwa fedha za Kitanzania zaidi ya Million mia sita (Tsh 603, 890,563.00/=) ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu.
Awali Kata hii haikuwa na Shule ya Sekondari, Ujenzi huu unahusisha ujenzi wa Jengo la Maabara, Jengo la TEHAMA, Jengo la Maktaba, Jengo la Utawala yakiwa katika hatua ya ukamilishaji na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa jengo la ghorofa ukiwa hatua ya msingi.
Ujenzi huu ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kunakuwa na fursa ya kupata elimu bora na za kutosha pasipo kikwazo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa