Na Mwandishi wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepongezwa kwa kukamilisha Ujenzi wa vyumba vya madarasa arobaini na nane (48) kwa ubora na wakati vilivyojegwa kwa kiasi cha fedha za Kitanzania Million mia tisa sitini (Tsh 960,000,000/=) kutokana na fedha za Mradi wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19
Yalisemwa hayo na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe siku ya Ijumaa Desemba 31, 2021 wakati akikabidhiwa miundombinu hiyo katika Shule ya Sekondari Buteko iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji mara ya baada ya kukamilika
Mkuu huyo wa Wilaya alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Ujenzi wa vyumba vya madarasa Nchi nzima huku akisema kukamilika kwa ujenzi huo kutaboresha kukua kwa viwango cha elimu Nchini
Mkuu huyo wa Wilaya alizipongeza kamati mbalimbali za Ujenzi zilizo shiriki huku akisema miundombinu hiyo itakuwa chachu na motisha kwa mazingira ya Ufundishaji na Ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi, Walimu na wanafunzi kuhakikisha wanalinda muundombinu hiyo ili kuweza kutumika kwa mda mrefu na kuwanufaisha wanafunzi walio wengi watakao kuwa wakijiunga na masomo ya Upili katika Manispaa hiyo
Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila akisoma Taarifa ya Mradi alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia Wanafunzi elfu mbili mia nne (2400) kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa wakati na kusoma kwa awamu moja kwa Shule za Sekondari zilizopo
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Buteko Ndugu. Dismas Nyakamwe alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuboresha huduma za jamii huku akisema bodi ya Shule ikishirikana na Wananchi watahakisha wanalinda miundombinu ya madarasa na kuwa manufaa kwa wanafunzi walio wengi
Wilaya ya Kigoma ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania billion mbili (Tsh 2,850,000,000) kutoka kwa Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu sekta ya Elimu na afya ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa sitini na tisa (69), ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika vituo Shikizi 6, na ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na ujenzi wa madarasa arobaini na nane Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Picha na video za vyumba vya madarasa Tembelea Maktaba ya Picha kwa tovuti www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa