Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Katika Kata ya Kipampa unaendelea kwa fedha za Kitanzania zaidi ya Million mia sita (Tsh 603, 890,563.00/=) ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa nane (8) kwa jengo la ghorofa unaendelea ukiwa hatua ya ujenzi wa nguzo na Sakafu ya Kwanza ambapo jengo hilo litakuwa na ghorofa tatu (03) na madarasa kumi na Sita (16) hadi kukamilika kwake.
Aidha Ujenzi wa majengo ya Maabara, TEHAMA, Maktaba, na Jengo la Utawala tayari yamekamilika.
Ujenzi huu ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kunakuwa na fursa ya kupata elimu bora na pasipo kikwazo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa