Na Mwandishi Wetu
Upasuaji wa kwanza kwa Mama mjamzito katika kituo cha afya cha Gungu umefanyika Leo January 5, 2023 Mara baada ya uzinduzi wa kuanza kwa huduma hiyo
Upasuaji huo umeanza Mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe kuzindua kuanza rasmi kwa huduma hiyo ya Upasuaji katika kituo hicho cha Afya cha Gungu
Akizindua huduma hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza na kushukuru Serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za afya katika Wilaya hiyo ikiwemo uboreshaji wa huduma na Ujenzi wa Majengo katika Kituo cha afya kipya cha Buhanda na uboreshaji wa huduma kituo cha afya cha Ujiji
Aidha amewataka Watumishi wa Afya kufanya kazi kwa weredi na kuonesha upendo kwa Wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu katika kituo hicho wakiwemo Wajawazito watakaokuwa wakipata huduma ya upasuaji mara baada ya uchungu pingamizi katika kipindi cha kujifungua
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashimu Mvogogo amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani imefanikisha Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara, Jengo la kufulia, jengo la wodi ya Wazazi na Upasuaji katika kituo hicho cha afya cha Gungu kwa gharama ya fedha za Kitanzania Millioni Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya Upasuaji pamoja na vifaa vya uhifadhi damu salama
Amesema Serikali imeendelea kufanya uboreshaji wa huduma katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuongeza damu kutokana na uwepo wa vifaa vya utunzaji damu salama
Amesema kupatikana kwa huduma hizo kutaondoa utoaji rufaa kwa Wagonjwa kuelekea katika hospitali ya Babtisti na Hospitali ya rufaa ya Maweni kupata huduma ya Upasuaji pamoja na kuongezewa damu
Nao baadhi ya Wananchi Waliohudhuria katika ufunguzi huo akiwemo Samsoni Nathani na Bi. Grace Nashoni wameipongeza Serikali kwa jitihada za uboreshaji na upatikanaji wa huduma bora za afya huku wakisema huduma hizo utahakikisha Usalama wa maisha ya Mama na Mtoto pindi Mjamzito anapojifungua
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa