Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeibuka Mshindi wa Sita (06) katika kundi la Halmashauri za Manispaa Nchini katika Mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka 2022 yanayoratibiwa kila Mwaka na Wizara ya Afya Nchini Tanzania
Manispaa hiyo imeibuka Mshindi wa nafasi hiyo huku jumla ya Halmashauri za Manispaa ishirini (20) zilishirikishwa katika Mashindano hayo
Aidha benki ya CRDB tawi la Kigoma Mjini nayo imeibuka Mshindi wa nafasi ya Sita (06) kwa afya na usafi wa Mazingira kati ya kundi la benki ishirini na tano (25) zilizoshiriki katika Mashindano hayo
Mashindano haya yamekuwa yakifanyika kwa lengo la kuinua hali ya Afya na Usafi wa Mazingira katika ngazi ya kaya na taasisi hivyo kusaidia katika kulinda na kuboresha afya ya jamii
Mashindano haya hufanyika kwa kuhusisha ngazi za Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali Nchini Tanzania na Kwa mwaka huu, mashindano haya yamehusisha Halmashauri zote nchini yakianzia katika ngazi ya Kijiji/Mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa na hatimaye Taifa
Vigezo vilivyozingatiwa wakati wa uhakiki wa mashindano hayo ni pamoja na; hali ya upatikanaji wa maji safi na salama, uwepo wa vyoo bora, udhibiti wa taka ngumu, udhibiti wa majitaka, usalama wa chakula, upendezeshaji wa maeneo, ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua, utunzaji wa maeneo ya maziko, usimamizi wa Sheria za Usafi, ubora wa huduma za kijamii na usafi katika maeneo ya umma.
Taarifa ya Matokeo inapatikana katika tovuti ya www.kigomaujijimc.go.tz na mitandao ya kijamii ya wizara ya Afya
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa