Na Mwandishi Wetu
Zoezi la Anwani za Makazi Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo March 21, 2022 limeanza kwa kuweka namba za Utambulisho wa Makazi, biashara na maeneo ya Umma katika Mitaa iliyopo kata ya Kitongoni katika Manispaa hiyo
Mitaa hiyo ambayo zoezi hilo limefanyika ni Mtaa wa Wafipa, Kabondo na Mnazi mmoja likihusisha Kamati ya uratibu ngazi ya Manispaa, Mtendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa na zoezi hilo linatarajia kuendelea katika Kata zingine ambapo Manispaa hiyo ina jumla ya Kata 19 na Mitaa 68 ya Kiutawala
Utambuzi na uwekaji wa Anwani za makazi Nchini unafanyika kwa kutoa namba ya anwani (namba ya jengo, au kiwanja), majina ya barabara au kitongoji na postikodi
kukamilika kwa zoezi hilo kila Mtanzania atakuwa na anwani halisi ya Makazi yatakayosaidia kila mtu kupatikana kirahisi, utambulisho wa watu, usajili wa biashara na mali na kuboreshwa kwa taarifa ya vizazi na vifo katika jamii
Aidha zoezi hilo pia litasaidia kufanyika kwa biashara mtandaoni ambapo Wafanyabiashara na wanunuzi watakuwa na uwezo wa kununua na kumfikishia mteja bidhaa, upatikanaji wa huduma za dharura kama vile polisi, huduma za zima moto kwa uharaka kutokana na uwepo wa anwani na taarifa kamili za kila mtu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizindua zoezi hilo kitaifa February 08, 2022 Jijini Dodoma aliwataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Nchini kusimamia kikamilifu na Kuhakikisha zoezi hilo linakamilika Mwezi Mei, Mwaka huu ili lilahisishe zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Mwezi August, 2022
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa