Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo Jana Julai 26, 2023 alisema uwekezaji wa bandari kwa sekta binafsi utaleta tija katika kuinua uchimi wa Watanzania
Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano ulioandaliwa na chama hicho ukihusisha Wakazi wa Mkoa wa Kigoma na Katavi katika kutoa elimu kuhusu mkataba wa ushirikiano wa uwekezaji na uendeshaji wa Bandari Nchini uliofanyikia Uwanja wa Mwaga Community centre Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Alisema lengo la Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kuisimamia Serikali katika Uendelezaji na uwekezaji katika Sekta binafsi kwa lengo la kukuza Uchumi wa Nchi na kuongeza ufanisi na tija katika bandari zilizopo Nchini
Alisema uwekezaji katika bandari kwa sasa ni kukuza uwezo katika kuhudumia na kuongeza Wateja kutoka Nchi jirani zinazotegemea kupitisha mizigo Nchini
Habari zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa